Libros importados hasta 50% OFF + Envío Gratis a todo USA   Ver más

menú

0
  • argentina
  • chile
  • colombia
  • españa
  • méxico
  • perú
  • estados unidos
  • internacional
portada Ujasusi Wa Kidola Na Kiuchumi (en Swahili)
Formato
Libro Físico
Idioma
Swahili
N° páginas
732
Encuadernación
Tapa Blanda
Dimensiones
22.9 x 15.2 x 4.1 cm
Peso
1.06 kg.
ISBN13
9789976993608

Ujasusi Wa Kidola Na Kiuchumi (en Swahili)

Yericko Nyerere (Autor) · 978-9976-9936-0-8 · Tapa Blanda

Ujasusi Wa Kidola Na Kiuchumi (en Swahili) - Nyerere, Yericko

Libro Físico

$ 36.00

$ 45.00

Ahorras: $ 9.00

20% descuento
  • Estado: Nuevo
Se enviará desde nuestra bodega entre el Miércoles 10 de Julio y el Jueves 11 de Julio.
Lo recibirás en cualquier lugar de Estados Unidos entre 1 y 3 días hábiles luego del envío.

Reseña del libro "Ujasusi Wa Kidola Na Kiuchumi (en Swahili)"

UTANGULIZI Naam. Ili mtu awe Afisa wa Idara ya Ujasusi yampasa awe mwenye akili zilizotulizana. Yaani, razini. Ndipo basi, pasi na kutafuna maneno, kitabu hiki ni mahususi hususan kwa wasomaji weledi. Kitabu hiki ni motifu, kinachoangazia masuala umuhimu ya ujasusi na jinsi yalivyo ya kipekee, kikitilia uzito umuhimu wake katika maisha ya wanadamu. Kutokana na upekee huo, taaluma ya ujasusi itumike kuleta ustawi katika jamii badala ya kudhuru kama ambavyo mashirkika mbalimbali ya ujasusi yamekuwa yakifanya kwa njia moja au nyingine, hii au ile. Ama kitabu hiki kinakusudiwa kutoa mwanga wa jinsi taaluma hiyo inavyopasa kuendeshwa pamoja na kuonesha uhalisia wa utendaji wake, kinyume na ilivyo kwa baadhi ya mashirika ambapo sasa imefikia hatua jasusi, kachero au afisa usalama kutangaza hadharani, "Unanijua mimi nani? Mimi ndimi, afisa usalama. Sichezewi!" Kwa lengo duni, ili kuwatisha watu kwa sifa za Mfalme Juha. Mintarafu, kitabu hiki ni bashraf kwa baadhi ya mataifa yanayoendelea kuhusiana na suala zima la ujasusi, mathalani ujasusi wa kidola wa Idara ya Usalama wa Taifa la Tanzania (TISS) na Ujasusi wa Kimataifa unaofanywa na mashirika kama MOSSAD la Israel katika harakati zake za kutimiza dhamira ya kutawala eneo zima la Mashariki ya Kati na dunia kwa ujumla. Zaidi ya hayo, kitabu hiki kinatoa maarifa pevu ya kijasusi ili kuelewa misingi ya ujasusi na umuhimu wake pamoja na kukamilisha shughuli zake mbali mbali. Mathalani kuna Ujasusi wa Kiushindani (Competitive Intelligence) ambao zaidi hutumika katika ulimwengu wa biashara na harakati waweza kuainishwa kama utaratibu wa kiufundi wa kupata habari nyeti za biashara na harakati za malengo, wateja, washindani, maadui, teknolojia na mazingira ya jumla ya harakati na biashara. Habari hizi zaweza kutoka kwa mtu yeyote au vyanzo vyovyote katika eneo husika. Ujasusi unatajwa kama ni taaluma ya pili kongwe duniani. Yaani, ulikuwapo tangu utanguni, ulimwengu ulipopata maarifa. Mashujaa katika vita vya kale wanasema kuwa ujasusi ni sehemu muhimu ya kimkakati, wakati wa vita. Kinachomuwezesha kamanda hodari kushambulia, kuteka na kufanya mambo yasiyo ya kawaida, yaliyo nje ya uwezo wa kawaida, ni ule ujuzi anaokuwa nao kabla ya pambano lenyewe. Na, ujuzi huo anaokuwa nao kabla, hautokani na uzoevu ama uhodari wa kufanya mahesabu, bali unatokana na taarifu za siri za adui ambazo hupatikana kutoka kwa watu wengine. Aidha, ujasusi umekuwa sehemu muhimu ya taasisi za kijeshi na kibiashara. Na pia, ujasusi ulikuwa na hadi leo umekuwa ni chachu ya harakati za Kanisa Katoliki. Punde taarifu zinapopatikana, husambazwa kwa usahihi na kwa wakati kwa watoaji maamuzi wa ngazi zote. Ujasusi wa Kiushindani (Competeteve Intelligence) ni ujasusi unaoshughulika zaidi na harakati za kibiashara ambao unatofautiana kidogo na ule wa serikali. Hata hivyo, serikali pia huuwa na idara ya ujasusi wa kibiashara. Ujasusi wa Kiushindani unafuata taratibu na maadili ya biashara ambayo hayafuatwi na taasisi za ujasusi unaohami serikali. Ujasusi wa Kiushindani haufanywi chini ya mwavuli wa kidiplomasia bali, una lengo zaidi la kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kuimarisha huduma na kukabili mikikimikiki ya ulimwengu kwa ajili ya kujipatia faida na ufanisi wa shughuli husika. Kadhalika, Ujasusi wa Kiushindani unatofautiana na ukachero mwingine wa kiserikali ambao huweza kukiuka au kupuuza sheria na taratibu za wengine. Nyuma ya pazia, mara nyingi, ujasusi hautazamwi kwa wema. Badala yake, ujasusi umeonekana kama shughuli isiyo na uhalali wa kimaadili au utu. Kwa ajili hiyo, kitabu hiki kinatoa changamoto kwa wajuzi na wajuvi wa taaluma hiyo, washiriki na watu wa kawaida kuonesha iwapo fani ya ujasusi itafanywa kitaalamu, inaweza kuwa ya muhimu kwa kurejea mifano ya wakongwe hasa MOSSAD (Israeli), CIA (Marekani), KGB (Urusi), M16 (Uingrereza) na wengineo, wameweza kutawala nyanja hio na kuweza kudhibiti kila sehemu kwa minajili ya kulinda na kuendeleza maslahi.............................................

Opiniones del libro

Ver más opiniones de clientes
  • 0% (0)
  • 0% (0)
  • 0% (0)
  • 0% (0)
  • 0% (0)

Preguntas frecuentes sobre el libro

Todos los libros de nuestro catálogo son Originales.
El libro está escrito en Swahili .
La encuadernación de esta edición es Tapa Blanda.

Preguntas y respuestas sobre el libro

¿Tienes una pregunta sobre el libro? Inicia sesión para poder agregar tu propia pregunta.

Opiniones sobre Buscalibre

Ver más opiniones de clientes